![]() |
Mwl. Elia Agrey |
SEHEMU YA PILI
Baada
ya kuangalia maana ya TOBA katika ile sehemu ya kwanza kama ambavyo tuliona
kuwa TOBA ni kugeuka kutoka katika jambo ambalo Mungu amelikataza
na kutenda lile ambalo Mungu ameliagiza kufanya au kutenda.
Katika sura hii nataka tuangalie UMUHIMU wa
TOBA kwa kanisa la sasa ambalo ni mimi na wewe uliyepata nafasi ya kusoma somo
hili
1.
TOBA
INAKUSOGEZA KARIBU NA MUNGU ZAIDI
Toba ya kweli inakusogeza karibu na Mungu na
kuyarudisha mahusiano kati ya mtu na Mungu ambayo yaliharibiwa na dhambi.Ule
uadui ambao dhambi iliuweka kati yako na Mungu unaondolewa na Mungu anakuwa
rafiki yako wa karibu.