SECOND CHANCE
Haki zote zimehifadhiwa. Si ruhusa kunakili, kuhifadhi kitabu hiki katika namna yoyote ya kielectroniki, wala kurekodi, labda kwa kuchukua point kwa ufupi, bila idhini ya maandishi ya mtunzi wa kitabu hiki.
(c) Elia Agrey
Simu: 0715-095013, 0689-441065, 0765-303146
Toleo la Kwanza: Julai 2014
Nakala 500
Kimepigwa chapa na;
AG - Press, Mbezi Beach,
P.0. Box 60411, Dar es salaam
Simu:0754-271144, 0715-271144
iii
YALIYOMO
Shukurani......................................................................................... iii
Utangulizi......................................................................................... iv
SURA YA KWANZA
* Kila mtu anakosea na anahitaji nafasi ya pili.................. 1
SURA YA PILI
* Ujihukumu kama Yuda au utubu kama petro................. 9
SURA YA TATU
* Si mpango wa Mungu wewe upotee................................. 15
SURA YA NNE
* Mungu ni Mungu wa msamaha............................................ 22
SURA YA TANO
* Unaitumiaje nafasi ya pili uliyopewa na Mungu?........ 29
SURA YA SITA
* Mungu anaweza kukusimamisha tena katika
nafasi yako....................................................................................... 36
Ukurasa
iv
SHUKURANI
Nina kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa neema zake na rehema zake maishani mwangu kwani amekuwa ni msaada wa karibu wakati wotePia namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuandika kitabu hiki cha pili chenye kichwa kinachosema SECOND CHANCE au kwa Kiswahili NAFASI YA PILI baada ya kuandika kitabu cha kwanza kinachosema OMBENI NANYI MTAPEWA
Ni maombi yangu na imani yangu kuwa kwa kupitia kitabu hiki utajifunza mambo mengi yatakayokusaidia katika kusimama tena na kuendelea na safari yako, iwe katika utumishi biashara, kazi, masomo na mambo mengine yote uliyokuwa ukiyafanya kwanza.
v UTANGULIZI
Ni imani yangu na maombi yangu kuwa kwa kupitia kitabu hiki utajifunza mambo mengi yatakayokusaidia katika kusimama tena na kuendelea na safari yako iwe katika utumishi, biashara, kazi, masomo na mambo mengine yote uliyokuwa ukiyafanya hapo kwanza.TABARUKU/DEDICATION
Kitabu hiki kimetolewa kwa heshima ya Mungu mwenyezi na kwa familia ya Agrey Mwambagi kama shukrani ya malezi na matunzo waliyonifanyia mpaka sasa, zaidi sana ni kwa kila mtu aliyekosea na anahitaji nafasi ya pili maishani mwake ili arejee mahali anapotakiwa kuwa.1
SURA YA KWANZA.
1. KILA MTU ANAKOSEA NA ANAHITAJI NAFASI YA PILIKatika maisha yetu ya kukaa hapa duniani kama wasafiri tunaosafiri kuelekea mbinguni ambako ndiko yaliko makao yetu ya milele tumekuwa tukifanya makosa mbalimbali ambayo kwa namna moja ama nyingine yameharibu mwelekeo wa safari tuliyonayo na kusababisha tukose nguvu ya kuendelea na safari yetu tuliyo nayo.
Inawezekana tumefanya makosa katika utumishi wetu ambao Mungu ametupa tumtumikie hapa duniani kwa kutoishi na kutenda sawa sawa na jinsi ambavyo Mungu anatutaka, au inawezekana tumekosea katika kazi ambazo kwa namna moja ama nyingine Mungu alitupatia tulipomuomba, lakini pia inawezekana umekosea katika biashara yako au umekosea katika mahusiano yako, ndoa yako na masomo yako, suluhisho la makosa yako haliko katika kukata tamaa na kurudi nyuma na kuacha kumtegemea Bwana na kumuomba Mungu suluhisho liko katika Mungu pekee. Watu wote tunakosea na tunahitaji nafasi ya pili hakuna mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke ambaye hakosei, wote tunakosea sio kwa makusudi au kwa kupanga kukosea la hasha ni sehemu tu ya maisha na Mungu anataka tujifunze kutokana na makosa.
Ukisoma Biblia katika kile kitabu cha Luka 15:11-19 tunaona habari ya mwana mpotevu na Biblia inasema 11 “…Akasema, Mtu mmoja alikuwa na wana wawili; 12 yule mdogo akamwambia babaye, Baba, nipe sehemu ya mali inayoniangukia. Akawagawia vitu vyake. 13 Hata baada ya siku si nyingi, yule mdogo akakusanya vyote, akasafiri kwenda nchi ya mbali; akatapanya
2
mali zake huko kwa maisha ya uasherati. 14 Alipokuwa amekwisha tumia vyote, njaa kuu iliingia nchi ile, yeye naye akaanza kuhitaji. 15 Akaenda akashikamana na mwenyeji mmoja wa nchi ile; naye alimpeleka shambani kwake kulisha nguruwe. 16 Akawa akitamani kujishibisha kwa maganda waliyokula nguruwe, wala hapana mtu aliyempa kitu. 17 Alipozingatia moyoni mwake, alisema, Ni watumishi wangapi wa baba yangu wanaokula chakula na kusaza, na mimi hapa ninakufa kwa njaa. 18 Nitaondoka, nitakwenda kwa baba yangu na kumwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako; 19 sistahili kuitwa mwana wako tena; nifanye kama mmoja wa watumishi wako…”
Tunaposoma habari ya mwana mpotevu, tunaona jinsi ambavyo alikosea kwa kutumia vibaya mali alizopewa na babaye kama urithi wake, sio kwamba alipewa kwa hiari ya baba yake lakini alipewa kwa kuomba apewe sehemu ya urithi wake na baba yao akawapa kila mmoja kadri alivyopenda.
Biblia inasema Yule mdogo baada ya kupewa urithi wake akaenda nchi ya mbali akatapanya mali kwa maisha ya uasherati, alikunywa na kulewa na kufanya anasa za kila namna kadri ambavyo mwili wake ulimuongoza, na kwa sababu ya mali aliyokuwa nayo kwa wakati ule aliyaona hayo ndiyo maisha hasa na ndio ujana kweli kweli. Watu wengi wamefanya makosa mbalimbali mara tu baada ya kupata Mali na nafasi Fulani katika jamii wakamsahau Mungu mioyoni mwao na kutenda maovu kwa kuongozwa na tamaa ya maisha ya anasa kama ambavyo mwana mpotevu alivyofanya. Ukiendelea kusoma Biblia katika kitabu hiki cha luka 15:14 Biblia inasema “…Alipokuwa amekwisha tumia vyote, njaa kuu iliingia nchi ile, yeye naye akaanza kuhitaji…”
3
Katika nchi ile ya ugenini baada ya kufanya anasa na uovu wa kila namna ile mali aliyokuwanayo haipo tena maana aliitumia kwa anasa bila kujua kuwa kesho itakuja na njaa itaingia katika nchi ile baada ya hali ya maisha kuwa ngumu akaona heri awe mtumwa ili ajipatie walau kula na kuishi, maisha yale ya anasa hayapo tena maana ameishi kwa kutapanya mali. Hakuna mtu aliye mjari tena na wale wote aliokuwa akitapanya nao mali hawapo tena kama ambavyo pia na wewe huwaoni tena wale watu walioshikamana nawe ulipokuwa na hali Fulani ya maisha na uliwaona ni msaada wako na watu wako wa karibu kweli kweli, ghafla hawapo tena akawa mpweke na peke yake mbele haoni njia wala mwelekeo, maisha yake yalibadilika ghafla na kuwa duni kama ambayo na wewe maisha yako yamebadilika ghafla kwa kukosea kwako katika jambo lolote maishani mwako.
Mstali ule wa 17 Biblia inasema “…17 Alipozingatia moyoni mwake, alisema, Ni watumishi wangapi wa baba yangu wanaokula chakula na kusaza, na mimi hapa ninakufa kwa njaa…” Baada ya kutathimini makosa aliyoyafanya akakumbuka kuwa yupo baba yake naye ana watumishi wengi chini yake wanaokula na kusaza, ndipo alipochukua uamuzi moyoni mwake wa kurudi kwa baba yake na kuomba msamaha na kuomba asiwe katika nafasi ya mwana tena bali awe nafasi ya utumwa kwa baba yake na asiwe mtumwa katika nchi ya ugeni.
Wewe sio mtu wa kwanza kukosea katika jambo lolote lile unaloona ya kwamba umekosea, wapo waliokosea kabla yako katika kosa hilo hilo kama lako, inawezekana umekosea katika utumishi wako, mahusiano yako, biashara yako, masomo yako na ukaona kana kwamba maisha hayaendi kabisa kama ulivyotamani yaende na unaona kabisa kukosea kwako ndiko kuliko kufikisha hapo, nataka nikutie moyo ya kwamba wewe sio mtu
4
wa kwanza kukosea, wapo wengi waliokosea kabla yako akiwemo mwana mpotevu. Uamuzi wako baada ya kukosea ndio kitu cha msingi kuliko kitu chochote kile na uamuzi unaouchukua baada ya kukosea ndio unaokufanya uyaimarishe maisha yako kwa upya baada ya kukosea au uendelee kuwa na maisha mabaya zaidi kwa sababu tu ulikosea kwanza.
Mwana mpotevu pamoja na kukosea kwake kwanza alichukua uamuzi wa busara na wa muhimu, Biblia inasema alipozingatia, maana yake aliyaona makosa yake na hakutaka kuendelea kukaa katika hali aliyokuwa nayo na aliona suluhisho pekee ni kurudi kwa baba yake na kumuambia babaye kuwa amekosa si tu kwake lakini na mbele za Mungu kwani yale alhiyoyatenda katika nchi ya ugeni hayakumpendeza baba yake pamoja na Mungu; ndio maana alisema nimekosa mbele zako (baba) na mbele za Mungu. Uamzi aliouchukua wa kurudi kwa babaye na kuomba msamaha uliyabadilisha maisha yake na hatimaye kuwa na maisha bora zaidi ya yale ya kwanza.
Tatizo si kukosea lakini tatizo ni unafanya nini baada ya kukosea
Watu wengi wamekuwa si wepesi wa kurudi na kurekebisha baada ya kukosea na hatimaye maisha yao yanakuwa na hali mbaya kuliko ile ya kwanza. Mungu anachotaka kwako na kwangu ni sisi kurudi na kuomba msamaha kwa yale tuliyokosea na tunaporudi na kuomba msamaha ndipo maisha yetu yanakuwa mazuri kuliko yale ya kwanza. Yesu alitoa mfano kwa wanafunzi wake ili kuwa fundisha kuwa kuna nafasi ya pili baada ya mtu kutumia vibaya ile nafasi ya kwanza aliyopewa katika jambo lolote lile, lakini pia.....
No comments:
Post a Comment