Friday, February 13, 2015

KUINGIA KATIKA AHADI YA MUNGU



KUINGIA KATIKA AHADI YA MUNGU PAMOJA NA NDUGU ZETU
Unaposoma Biblia habari za wana wa Yakobo aliyeitwa Israel mzao wa Isaka aliyepewa Ibrahim kwa ahadi ya Mungu unaona jinsi ambavyo Mungu alimuahidia Ibrahim mambo mazuri yatakayotokea kwake na kwa uzao wake na jinsi atakavyo wapa uzao wake baada yake kuingia katika nchi ya ahadi iliyo jaa maziwa na asali na kila mema yatokayo katika nchi.Ibrahim akafa pasipo kuiona ile ahadi Yakobo pia vivyo ivyo pamoja na Isaka wakafa pasipo kuiona ile ahadi,lakini Mungu kwa jinsi alivyomuaminifu katika kutimiliza ahadi zake na asivyo mwepesi wa kusahau alichokisema akawatimilizia uzao wa Ibrahimu ile ahadi aliyoisema kwa Ibrahim ya kuwapa nchi ya Kaanani iliyojaa maziwa na asali yaani kila mema yatafutwayo na watu wote wa duniani.
Safari ya kuelekea kuipata ile ahadi ilianzia kutoka nchi ya Misri ambako hawa watu walikaa katika nchi ya ugeni kwa muda wa miaka Zaidi ya 400 wakitumikishwa katika utumwa wa namna nyingi kama ambavyo Mungu alivyosema kwa Ibrahim ya kuwa watakaa katika nchi ya ugeni lakini baada ya hapo atawatoa katika mateso yao kwa mkono mkuu.

Pamoja na kwamba Mungu alimuahid Ibrahim kuwa atawatoa watu wake katika utumwa na kuwapa nchi iliyo bora Zaidi si kila aliyetoka katika ule utumwa wa Misri na kuona ishara miujiza na maajabu mengi ambayo Mungu aliyatenda kwao aliweza kuingia katika Nchi ya AHADI bali ni watu wale tu waliokuwa na Imani na Mungu katika kile alichokisema ndio walioweza kuingia katika nchi ile ya ahadi ambao ni Yoshua na Kalebu na kizazi chao,wote waliotoka Misri utumwani hawakuingia kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao na kutokuamini kwao,waliona ISHARA waliona MAAJABU waliona MIUJIZA lakini hawakuingia katika nchi ya ahadi.

Waebrania 4:1 “…Basi, ikiwa ikaliko ahadi ya kuingia katika raha yake, na tuogope, mmoja wenu asije akaonekana ameikosa…”
Mwandishi wa kitabu hiki cha Waebrania anajaribu kutupa tahadhari watu wa kipindi hiki na watu wa nyakati hizi za sasa maana kwa jinsi alivyoandika maneno haya inaonyesha wazi kuwa ni mtu aliyepata uzoefu na anayejua nini kilitokea kwa kizazi kile ambacho hakikumuamini Mungu katika yale maneno aliyoyasema kwao.

Ukiyatafakari kwa makini haya maneno unaona ya kuwa bado ipo AHADI ambayo Mungu ametoa kwa watu wote wa kizazi hiki ya kuingia katika RAHA YAKE Mungu si wana wa Israeli tu bali kwa watu wote na ahadi iyo inapatikana kwa kila mtu amwaminiye Yesu Kristo kama Bwana na mwokozi wa maisha yake sasa ni uamuzi wa watu kuamini au kutokuamini lakini angalizo linatolewa kwa wale wasio amini ili kile kilichowatokea watu wa kizazi kile kisije kikatokea kwa watu wa kizazi hiki cha sasa maana kutokuamini kulifuta matumaini yao ya kuingia katika ahadi ya Mungu kwao licha ya kuona ishara na miujiza mingi kwao.Unaweza ukaona ishara na miujiza mingi Mungu akifanya kwako lakini isikusaidie kama ambavyo haikuwasaidia wana wa Israel katika kuingia katika ahadi ya Mungu hasa kwa kutokumuamini Mungu na kuwa wagumu wa mioyo wapendao  mabaya na wachukiao mazuri.
 Kwa iyo ili wewe na jamaa zako msiingie katika orodha ya watu waikosao ahadi ya kuingia katika raha ya milele katika Kristo Yesu inakupasa kumuamini Mungu na kutenda mema na kuyaacha mabaya yote na yaliyo maovu yote.
Paulo hakuwa anaongea na watu wasio wapendwa alikuwa anaongea na waongofu wa mwanzo akiwapa namna iwapasavyo kutenda na kufanya.Ni muhimu ukajua umuhimu wa onyo hili ambalo mtumishi wa Mungu amelitoa kwa watu waaminio ili wasije kuikosa ahadi iliyotolewa na Yesu Kristo kwa iyo suala sio tu kusema umeokoka bali ni kuishi maisha ya Imani na Utakatifu katika Kristo ili usiikose ahadi ya Mungu kwa watu wake wampendao.
Waebrania 3:13-19
13 “…Lakini mwonyane kila siku, maadamu iitwapo leo; ili mmoja wenu asifanywe mgumu kwa udanganyifu wa dhambi.
 14 Kwa maana tumekuwa washirika wa Kristo, kama tukishikamana na mwanzo wa uthabiti wetu kwa nguvu mpaka mwisho;
 15 hapo inenwapo, Leo, kama mtaisikia sauti yake, Msifanye migumu mioyo yenu, Kama wakati wa kukasirisha.
 16 Maana ni akina nani waliokasirisha, waliposikia? Si wale wote waliotoka Misri wakiongozwa na Musa?
 17 Tena ni akina nani aliochukizwa nao miaka arobaini? Si wale waliokosa, ambao mizoga yao ilianguka katika jangwa?
 18 Tena ni akina nani aliowaapia ya kwamba hawataingia katika raha yake, ila wale walioasi?
 19 Basi twaona ya kuwa hawakuweza kuingia kwa sababu ya kutokuamini kwao…”

Ukiangalia kwa umakini na utaratibu hii mistari unaona jinsi ambavyo Mungu yuko serious katika kile alichokisema na anafuata Neno lake alilolisema kwa watu wake kwa ivyo ni muhimu kufanya alivyosema ili upate alichosema utapata.
Huu ni utaratibu ambao wewe kama mwamini inatakiwa uwe nao na uishi kila siku ukiufuata huo na sio wewe tu kuufuata na kufurahia kuufuata bali kuwahimiza na wale wasioufuata waufuate ili wasije kupotea,unapoona mwenzio hafuati utaratibu ambao Mungu amesema ni vyema ukamrekebisha na kumuonyesha jinsi impasavyo kutenda na kufanya na huu ni utaratibu wa kibiblia kabisa kama tunavyosoma ule mstari wa 13  “…Lakini mwonyane kila siku, maadamu iitwapo leo; ili mmoja wenu asifanywe mgumu kwa udanganyifu wa dhambi…”

Yuda 1:23 "...na wengine waokoeni kwa kuwanyakua katika moto; na wengine wahurumieni kwa hofu, mkilichukia hata vazi lililotiwa uchafu na mwili..."

Ivyo basi ili na sisi tusipatwe na kile kilichowapata wao imetupasa kutofanya kile walichofanya wao yaani kuto kumwamini kwao Mungu na kutenda yaliyo maouvu

19 “…Basi twaona ya kuwa hawakuweza kuingia kwa sababu ya kutokuamini kwao…”




No comments:

Post a Comment