MAOMBI

TAFSIRI YA MAOMBI


Maombi ni neno lenye tafsiri mbalimbali na kila mtu hulielezea vile anavyopata ufunuo kwa wakati huo, upana wake umepelekea watu mbalimbali kuwa na mitazamo tofauti tofauti juu ya uhalisia wa maombi yenyewe.

Maombi yamejikita katika nguzo kuu tatu, ambazo ni

1.  Muombaji [mtu/mwanadamu],
2. Muombwaji [anayeombwa 
3.     Kipeleka maombi [mawasiliano] 

Maombi yanawasilishwa na pande mbili tofauti zinazotofautiana kiuwezo, ni lazima upande mmoja uwe na nguvu ya kutimiza mahitaji ya upande wa pili, mfano: mwanadamu anapoamua kumuomba Mungu ampe ulinzi wa maisha yake wakati wote au anapoomba rafiki yake amsaidie kifedha, ili kupata majibu ya maombi yake kunahitajika uwezesho wa kimawasiliano baina ya hizi pande mbili.
Ili maombi yaweze kuwa maombi ni lazima kuwepo na mapatano au makubaliano baina ya hizi pande kuu mbili zinazotofautiana kwa namna moja ama nyingine kiroho, kimwili, kiuchumi, kifikra, kielimu, kisiasa, kijamii na kadharika.

Tafsiri rahisi za maombi ni:-

Maombi ni kuhitaji msaada katika ulimwengu wa roho ili kutatua mahitaji yaliyopo katika ulimwengu wa Mwili. Ni ile hali ya kufungua mioyo yetu kwa Mungu ili akutane na mahitaji yetu, mara zote maombi hayamshushi Mungu chini duniani bali yanaifanya mioyo yetu inyenyekee na kupata kibali mbale zake.

Maombi ni kumpa Mungu kibali ama leseni cha kulitimiza kusudi lake kwa kupitia mwanadamu aliyemuumba hapa duniani, kibali hiki humfanya Mungu apitishe vitu vyake hapa duniani kwa kupitia mwanadamu.

Maombi ni mawasiliano yaliyoko kati ya Mungu mtakatifu na mwanadamu aliyeko duniani kwa njia ya Yesu Kristo na kwa msaada wa Roho mtakatifu.

Kama mawasiliano yalivyo na umuhumu hapa duniani katika kufanikisha mipango na mikakati ya kimaisha katika jamii za aina zote, ndivyo maombi yalivyo na umuhimu katika kuufurahia uhusiaono wetu na Mungu hapa duniani. Ili tuwe na nguvu rohoni na kuishi maisha ya utakatifu na ya kumpendeza Mungu kila wakati tunatakiwa kuwa na uhusiano binafsi ulio halisi na baba yetu wa Mbinguni.

Huwezi kumtenganisha mkristo na maombi, hakuna maombi yasiyokuwa na njia au namna ya kuyawasilisha na kuyapeleka kwa Yule umuombaye ambaye ni Kristo Yesu kwa kusaidiwa na Roho Mtakatifu.

Ili mkristo aweze kuvuta hewa safi na yenye usalama kwa maisha yake yote ya rohoni inampasa awe na muda wa kutosha wa kuzungumza na Mungu wake kila wakati na kuyatenda yote anayoagizwa kwa wakati muafaka [hayo ni maombi]

Tumeambiwa kuwa “Tusijisumbue kwa Neno lolote, bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushuru, haja zenu na zijulikane na Mungu (Wafilipi 4:6);

Kwa kusisitiza anasema:-
“Basi kabla ya mambo yote Mungu anataka dua na sala na maombezi na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote [1 Timotheo 2:1]


Hivyo tuungane pamoja katika kuliombea kanisa na taifa la Tanzania kwa ujumla.

tushirikishe dondoo za maombi kwa ku comment au kutuandikia maoni kwenye link yetu hapo chini:- 
Mungu awe nasi tangu sasa na hata milele, Amina.

No comments:

Post a Comment