DIRA:
kuwafikia watu wengi kwa kadiri iwezekanavyo kutoka katika makabila yote, lugha zote na mataifa mbalimbali kwa neno la Mungu
DHAMIRA
Dhamira yetu ni kuihubiri injili na kufundisha kweli ya neno la mungu kwa mfumo rahisi na wa kueleweka, ili injili ya Kristo iwafikie mataifa yote kama agizo kuu linavyosema “Enendeni ulimwenguni mwote mkawafanye mataifa kuwa wanafunzi wangu. (Mathayo 28:19-20)
KUANZA KWA HUDUMA
Huduma hii ilanzishwa mwaka 2005
ikiwa na jumla ya washiriki kumi na mbili, wengi wao ni waalimu na wahubiri wa
injili, wengine ni waimbaji na waombaji, lengo kuu la huduma hii ni kuliimarisha
kanisa yaani mwili wa kristo kwa kuifundisha kweli ya Neno la Mungu kwa usahihi
na umahiri mkubwa. Hii ni kutokana na mwili wa kristo hasa makanisani kukosa
wahudumu wenye sifa na ujuzi sahihi wa elimu ya Neno la Mungu katika viwango
vinavyotakiwa.
MAANA YA JINA
Boanerge ni jina walilopewa
Yakobo na Yohana baada ya Yesu Kristo kuwachagua wanafunzi wake kumi na wawili
na kuwapa majina (linatoka katika kitabu cha Marko 3:17 “Na Yakobo mwana wa zebedayo na
Yohana nduguye yakobo akawapa jina la Boanerge maana yake wana wa Ngurumo”).
Kwa kuwa Yeye ndiye aliyewaumba na kuijua asili ya kila kitu akaona hilo jina
linawafaa hao yaani BOANERGE ni jina la Kigiriki lenye maana ya WANA WA
NGURUMO” ambapo kwa tafsiri ya sasa hili jina linamaanisha wahubiri wa injili
wenye moto na nguvu ya Mungu walio jasiri kuihubiri kweli ya Mungu bila kujali
hali, mazingira na kipingamizi chochote.
Kutokana na thamani ya hili jina,
ndipo neno la huduma likawa ni Mathayo 10:5-8 wenye sifa zifuatazo, pozeni
wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni
bure. Unao-endana haswa na jina la huduma yaani “WANA WA NGURUMO”
MSINGI WA HUDUMA:
“…. Na katika kuenenda kwenu,
hubirini mkisema, ufalme wa mbinguni umekaribia, pozeni wagonjwa, fufueni wafu,
takaseni wenye ukoma, toeni pepo, mmepata bure, toeni bure.” [Mathayo 10: 5-8]
Neno kuu la huduma ni ile Mathayo
10:5-8, na ukianzia ule mstari wa tano anasema “Hao thenashara Yesu aliwatuma
akisema, katika njia ya mataifa msiende, wala katika mji wowote wa samaria
msiingie. 6 Afadhari shikeni njia kuwaendea kondoo waliopotea wa
nyumba ya Israeli….”
Nyumba ya Israel kwa karne ya
sasa ni watu wote walio-okoka ambao wanaitwa mwili wa Kristo, haijalishi upo
katika dhehebu gani, maadam umeokoka wewe ni nyumba ya Israel kibiblia. Sasa
hao ndio tulioitwa kwao, yaani tuwafundishe kweli ya neno la Mungu, na
kuwahubiria ijnili tukisema “ufalme wa
mbinguni umekaribia, tupoze wagonjwa, tufufue wafu, tutakase wenye ukoma, tutoe
pepo maana tumepata bure ni sharti tutoe bure” [Mathayo 10: 7-8] ndio maana
wengi wa wahudumu wa huduma hii ni waalimu na wahubiri, ingawa wapo wengine
waimbaji, waombolezaji, wachungaji, wainjilisti na mitume.
Tunahubiri na kufundisha neno la
Mungu kwa njia mbalimbali kama mikutano ya hadhara, semina za ndani,
makongamano, matamasha, mikesha ya maombi, umisheni na uhamasishaji wa
kimaendeleo kwa watu wote. Pia tunatumia machapisho mbalimbali kama vitabu, vipeperushi
barua pepe, kwa njia ya mitandao, CD & DVD na kwa mfumo wowote wa
ki-electroniki ili injili iyafikie mataifa yote.
No comments:
Post a Comment