KUINGIA
KATIKA AHADI YA MUNGU PAMOJA NA NDUGU ZETU
Unaposoma Biblia habari za
wana wa Yakobo aliyeitwa Israel mzao wa Isaka aliyepewa Ibrahim kwa ahadi ya
Mungu unaona jinsi ambavyo Mungu alimuahidia Ibrahim mambo mazuri yatakayotokea
kwake na kwa uzao wake na jinsi atakavyo wapa uzao wake baada yake kuingia
katika nchi ya ahadi iliyo jaa maziwa na asali na kila mema yatokayo katika
nchi.Ibrahim akafa pasipo kuiona ile ahadi Yakobo pia vivyo ivyo pamoja na
Isaka wakafa pasipo kuiona ile ahadi,lakini Mungu kwa jinsi alivyomuaminifu
katika kutimiliza ahadi zake na asivyo mwepesi wa kusahau alichokisema
akawatimilizia uzao wa Ibrahimu ile ahadi aliyoisema kwa Ibrahim ya kuwapa nchi
ya Kaanani iliyojaa maziwa na asali yaani kila mema yatafutwayo na watu wote wa
duniani.
Safari ya kuelekea kuipata ile ahadi ilianzia kutoka nchi ya Misri
ambako hawa watu walikaa katika nchi ya ugeni kwa muda wa miaka Zaidi ya 400 wakitumikishwa
katika utumwa wa namna nyingi kama ambavyo Mungu alivyosema kwa Ibrahim ya kuwa
watakaa katika nchi ya ugeni lakini baada ya hapo atawatoa katika mateso yao
kwa mkono mkuu.
Pamoja na kwamba Mungu alimuahid Ibrahim kuwa atawatoa watu wake
katika utumwa na kuwapa nchi iliyo bora Zaidi si kila aliyetoka katika ule
utumwa wa Misri na kuona ishara miujiza na maajabu mengi ambayo Mungu
aliyatenda kwao aliweza kuingia katika Nchi ya AHADI bali ni watu wale tu
waliokuwa na Imani na Mungu katika kile alichokisema ndio walioweza kuingia
katika nchi ile ya ahadi ambao ni Yoshua na Kalebu na kizazi chao,wote
waliotoka Misri utumwani hawakuingia kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao na
kutokuamini kwao,waliona ISHARA waliona MAAJABU waliona MIUJIZA lakini
hawakuingia katika nchi ya ahadi.
Waebrania
4:1 “…Basi, ikiwa ikaliko ahadi ya kuingia katika raha yake, na tuogope, mmoja
wenu asije akaonekana ameikosa…”
Mwandishi wa kitabu hiki cha
Waebrania anajaribu kutupa tahadhari watu wa kipindi hiki na watu wa nyakati
hizi za sasa maana kwa jinsi alivyoandika maneno haya inaonyesha wazi kuwa ni
mtu aliyepata uzoefu na anayejua nini kilitokea kwa kizazi kile ambacho
hakikumuamini Mungu katika yale maneno aliyoyasema kwao.
Ukiyatafakari kwa makini
haya maneno unaona ya kuwa bado ipo AHADI ambayo Mungu ametoa kwa watu wote wa
kizazi hiki ya kuingia katika RAHA YAKE Mungu si wana wa Israeli tu bali kwa
watu wote na ahadi iyo inapatikana kwa kila mtu amwaminiye Yesu Kristo kama
Bwana na mwokozi wa maisha yake sasa ni uamuzi wa watu kuamini au kutokuamini
lakini angalizo linatolewa kwa wale wasio amini ili kile kilichowatokea watu wa
kizazi kile kisije kikatokea kwa watu wa kizazi hiki cha sasa maana kutokuamini
kulifuta matumaini yao ya kuingia katika ahadi ya Mungu kwao licha ya kuona
ishara na miujiza mingi kwao.Unaweza ukaona ishara na miujiza mingi Mungu
akifanya kwako lakini isikusaidie kama ambavyo haikuwasaidia wana wa Israel
katika kuingia katika ahadi ya Mungu hasa kwa kutokumuamini Mungu na kuwa
wagumu wa mioyo wapendao mabaya na
wachukiao mazuri.
Kwa iyo ili wewe na jamaa
zako msiingie katika orodha ya watu waikosao ahadi ya kuingia katika raha ya
milele katika Kristo Yesu inakupasa kumuamini Mungu na kutenda mema na kuyaacha
mabaya yote na yaliyo maovu yote.
Paulo hakuwa anaongea na
watu wasio wapendwa alikuwa anaongea na waongofu wa mwanzo akiwapa namna
iwapasavyo kutenda na kufanya.Ni muhimu ukajua umuhimu wa onyo hili ambalo
mtumishi wa Mungu amelitoa kwa watu waaminio ili wasije kuikosa ahadi
iliyotolewa na Yesu Kristo kwa iyo suala sio tu kusema umeokoka bali ni kuishi
maisha ya Imani na Utakatifu katika Kristo ili usiikose ahadi ya Mungu kwa watu
wake wampendao.
Waebrania
3:13-19
13
“…Lakini mwonyane kila siku, maadamu iitwapo leo; ili mmoja wenu asifanywe
mgumu kwa udanganyifu wa dhambi.
14 Kwa maana tumekuwa washirika wa Kristo,
kama tukishikamana na mwanzo wa uthabiti wetu kwa nguvu mpaka mwisho;
15 hapo inenwapo, Leo, kama mtaisikia sauti
yake, Msifanye migumu mioyo yenu, Kama wakati wa kukasirisha.
16 Maana ni akina nani waliokasirisha,
waliposikia? Si wale wote waliotoka Misri wakiongozwa na Musa?
17 Tena ni akina nani aliochukizwa nao miaka
arobaini? Si wale waliokosa, ambao mizoga yao ilianguka katika jangwa?
18 Tena ni akina nani aliowaapia ya kwamba
hawataingia katika raha yake, ila wale walioasi?
19 Basi twaona ya kuwa hawakuweza kuingia kwa
sababu ya kutokuamini kwao…”
Ukiangalia kwa
umakini na utaratibu hii mistari unaona jinsi ambavyo Mungu yuko serious katika
kile alichokisema na anafuata Neno lake alilolisema kwa watu wake kwa ivyo ni
muhimu kufanya alivyosema ili upate alichosema utapata.
Huu ni utaratibu
ambao wewe kama mwamini inatakiwa uwe nao na uishi kila siku ukiufuata huo na
sio wewe tu kuufuata na kufurahia kuufuata bali kuwahimiza na wale wasioufuata
waufuate ili wasije kupotea,unapoona mwenzio hafuati utaratibu ambao Mungu
amesema ni vyema ukamrekebisha na kumuonyesha jinsi impasavyo kutenda na
kufanya na huu ni utaratibu wa kibiblia kabisa kama tunavyosoma ule mstari wa
13 “…Lakini
mwonyane kila siku, maadamu iitwapo leo; ili mmoja wenu asifanywe mgumu kwa
udanganyifu wa dhambi…”
Yuda 1:23 "...na wengine waokoeni kwa kuwanyakua katika moto; na wengine wahurumieni kwa hofu, mkilichukia hata vazi lililotiwa uchafu na mwili..."
Ivyo basi ili na sisi
tusipatwe na kile kilichowapata wao imetupasa kutofanya kile walichofanya wao
yaani kuto kumwamini kwao Mungu na kutenda yaliyo maouvu
19
“…Basi twaona ya kuwa hawakuweza kuingia kwa sababu ya kutokuamini kwao…”