Na: ERASTO KIBIKI
Katika biblia neno “wito” lina maana kubwa sawa na maana
yake katika lugha ya kila siku. Maana
hiyo pia inahusika kama biblia inasema habari za wito wa Mungu kwa watu
binafsi, ingawa maana nyingine zina alama nyingine za matumizi ya mafundisho ya
kidini.
Mungu anaita watu
katika maana ya kuwaamuru au kuwakaribisha, kama Isaya anavyoelezea jinsi Mungu
alivyoita na watu hawakuitika alivyonena na watu hawakusikiliza; anasema “Mimi
nitawaandikia kuuawa kwa upanga na ninyi nyote mtainama ili kuuawa kwa
kuchinjwa, kwa sababu NILIPOITA HAMKUITIKA, NILIPONENA HAMKUSIKIA; bali
mlitenda yaliyo mabaya machoni pangu, mlichagua mambo nisiyoyafurahia” [Isaya
65:12].
Hapa tunaona hawa watu
walifanya uchaguzi binafsi na kuukataa wito wa Bwana juu ya maisha yao, kisha
wakachagua mambo yasiyomfurahisha Mungu na wakaishia kuuawa na kuchinjwa.
Ndivyo ilivyo na kwetu hata sasa, mara nyingi wito halisi una upinzani mkubwa
sana. Kupandishwa cheo kazini au kupata kazi Fulani inaweza ikawa ni kuanguka
kwako katika wito ulioitiwa na kukusababisha uzichague njia zako mwenyewe na si
njia za Bwana.
Pia Yeremia anaandika
kuwa “Na
sasa kwa sababu mmezifanya kazi hizi zote asema BWANA, nami nikasema nanyi,
nikiamka mapema na kunena, lakini hamkusikia; NAMI NIKAWAITA WALA HAMKUITIKIA”
[Yeremia 7:13]
Hawa watu wamezifanya
kazi zao wenyewe, yaani wametimiza kusudi la kuishi kwao duniani bila ya Mungu
kuhusika, wamefanya yote kwa matakwa yao wenyewe,kisha Mungu akasema nao,
akiamka mapema sana na kunena habari za WITO WALIOITIWA na kusudi la kuishi
kwao duniani, na ya kuwa wageuke na kuziacha njia zao mbaya na kumuelekea Mungu
wao milele lakini HAWAKUSIKIA, na walipoitwa HAWAKUITIKA.
Mungu anakuita hata
sasa, anataka urudi kwenye asili yako, uenende kama ulivyoitwa, wewe umeitwa
uwafundishe watu KWELI ya Neno la Mungu, badala ya kwenda ulikoitwa, umejikuta
ukiwa BANK Teller au Mhasibu na kufungiwa kwenye kachumba ukihesabu pesa wakati
mamilioni ya watu wanaelekea JEHANAMU kwa kukataa kuishi kama ulivyoitwa.
“… Mwenende kama
inavyoustahili WITO WENU MLIOITIWA, kwa unyenyekevu wote na upole, kwa
uvumilivu, mkichukuliana katika upendo, na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho,
katika kifungo cha Amani” [Efeso 4:1-3]
Zaidi ya hayo Mungu
ANAWAITA watu katika maana ya KUWATEUA na KUWAONGOZA kwa kadiri ya makusudi
yake maalumu.
Isaya 43:1 inasema “Lakini
sasa, BWANA aliyekuhuruku, Ee yakobo, Yeye aliyekuumba Ee Israeli asema hivi;
Usiogope maana nimekukomboa; NIMEKUITA KWA JINA LAKO, wewe u wangu”
hapa tunaona Mungu akiwaita watu na kuwateua wawe wake, anawaongoza na kuwapa
mwelekeo maalumu wa maisha.
Ukijua kuwa duniani tu
wapitaji na wasafiri tusiokuwa na makao ya kudumu, utajua kuwa haikupasi kuishi
vile unavyotaka wewe bali unapaswa kutenga muda na kulitafuta kusudi la kuishi
kwako na hapo ndipo utakapoenda kama wito wako ulivyoitiwa.
Isaya
46:11 inasema “Nikiita ndege mkali
kutoka mashariki, mtu wa shauri langu toka nchi iliyombali; Naam, NIMENENA,
NAMI NITATEKELEZA; NIMEKUSUDIA, NAMI NITAFANYA” asema Bwana wa
Majeshi.
Mungu amekuitia kusudi
maalumu la kuishi kwako naye amenena kuwa ATATEKELEZA, na amekusudia kukuita hivyo ATAFANYA lile
alilokuitia. Hautatembea peke yako katika huo wito na hilo kusudi uliloitwa;
Mungu yupo nawe, songa mbele utafika.
Hosea 11:1 anaelezea kuwa “Israeli
alipokuwa mtoto, naalikuwa nikimpenda, NIKAMWITA mwanangu atoke Misri”
hapa Mungu alimpenda Israeli tangu utoto wake na AKAMWITA ili aliishi kusudi la
KUITWA kwake. Lakini mstari wa pili wa hii hosea 11 unasema hivi “kadiri
WALIVYOWAITA ndivyo walivyoondoka na kuwaacha; waliwatolea dhabihu mabaali na
kuzifukizia uvumba sanamu za kuchonga”
Kumbe unaweza ukawa
unaukataa wito wa Mungu maishani kwa sababu kuna watu au vitu vya kidunia
vikikuita na kuuchukua muda wako wote na hatimaye maisha yako, kuna watu
wameitwa na kuvutwa na MISHAHARA, PESA, BIASHARA, NDOA, KAZI n.k
Ni nini kilichokufanya
uukatae WITO ulioitwa? Hicho ndicho kilichokuita, nawe umekifuata na kukiabudu.
Ndio maana unashindwa kurudi kwenye kusudi la maisha yako.
“Kwa Imani Ibrahimu
ALIPOITWA aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi, akatoka
asijue aendako” [Ebrania11:8]
Kukubali kutoka hapo
ulipo na kwenda mahali unapoambiwa uende na wewe hupajui kisha ukaanza safari
ya kwenda, hapo ndipo tunaposema UMEITIKA NA UMEUKUBALI WITO WAKO. Wengine
wameitwa wakae Madhabahuni lakini wao wapo maofisini, wengine wameitwa kwenye
biashara na kwenye uongozi lakini wapo madhabahuni. Hii inaonyesha kuwa
KUUJUA WITO ulioitwa unapaswa kuwa na
utulivu wa kina mbele za Mungu.
Mtume Paulo anaelezea
uhakika wa kuitwa kwake kwenda Makedonia kuihubiri injili akisema “Basi
alipokwisha kuyaona yale maono, mara tukataka kutoka kwenda Makedonia, kwa kuwa
TULIONA HAKIKA ya kwamba MUNGU AMETUITA tuwahubiri habari njema” [Matendo
16:10]. Uhakika huu ulitokana na maono ya Mungu kwao, nasi imetupasa
kukaa magotini pa Mungu aliyehai na kwenda katika njia zake milele.
Katika maana ya juu
zaidi, Mungu anapowaita watu mbalimbali katika kazi yake huwa ANAWAITA kwa
kuwapa WOKOVU wake na kuwafanya wawe wake kabisa.
Wakristo ni watu
walioitikia WITO wa Mangu katika injili …..
Itaendelea………………………….