Monday, September 22, 2014

MWITE YESU WAKATI WOTE

Katika maisha usiogope kumwita Yesu, mwambie akuokoe ili usizame katika tamaa, anasa na udanganyifu wa mali za hapa duniani hata ukaipoteza nafsi yako ya thamani. nasisitiza tena, jiponye nafsi yako nawe ukaishi milele na Bwana katika ile mbingu mpya na nchi mpya aliyotuandalia; maana alisema 

"Naenda kwa Baba kuwaandalia makao, ili nilipo Mimi nanyi muwepo, na tazama Maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake, Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao" Ufunuo 21:1-9

Makao yamesha andaliwa na yanaendelea kuandaliwa, tujiandae maana wakati tusioudhani parapanda italia, wafu watafufuliwa na sisi sote tutamlaki Bwana mawinguni pamoja na mwaliko wa watakatifu, HAKIKIKISHA UNAKUWA MIONGONI MWA WATEULE kwa kuutunza utakatifu na kuokoka hali ungali hapa duniani.

No comments:

Post a Comment